
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa,Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George, mmoja kati ya waasisi wa Taifa la Tanzania amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu amethibitisha kutokea kwa kifo cha Sir. George na kusema kuwa amefariki leo saa kumi na dakika arobaini za jioni.
Sir. George Kahma , ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru mnamo miaka ya 1950, hadi kujitawala mwaka 1961.
Enzi za uhai wake Sir. George alishawahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Mungu ampumzishe mahali pema peponi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment