March 18, 2017

Image result for tundu lisu ashinda urais tls

Wakili msomi Mhe. Tundu Lissu ameshinda Urais wa Chama cha wanasheria nchini (TLS) kwa kupata kura 1,411 kati ya kura 1,682 zilizopigwa, sawa na ushindi wa 88% ya kura zote.

Katika mawasiliano na Lissu amethibitisha ushindi huo na kusema kwa kifupi "Nimeshinda Urais TLS, ushindi huu uende kwa watanzania wote, na kwa wote mlioonewa ambao mpo mahabusu na magerezani".

President: Tundu Lissu.
Vice President: Godwin Ngwilimi
HT: Magai

List of Council Members.
1. Jeremiah Mtobesya
2. Gida Lambaji
3. Hussein Mtembwa
4. Aisha Sinda
5. Steven Axweso
6. David Shilatu
7. Daniel Bushele.

-----Jinsi zoezi zima la Uchaguzi wa TLS lilivyokuwa-----
Ni asubuhi iliyo njema kabisa ndani ya Jiji la Arusha Mjini hali ya utuvuli na amani imetawala ambapo siku ya leo mawakili wasomi wataandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya wa Tanganyika Law Society (TLS )

Jana baada wagombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Tanganyika Law Society kujieleza na kuomba kura. Zoezi la kupiga litafanyika siku ya leo Jumamosi kuanzia majira ya Saa 06.00 hadi saa tatu baada ya hapo zoezi la kupiga kura kukamilika matokeo ya uchaguzi yatatangazwa rasmi.

Wagombea nafasi ya Uraisi wa TLS
1. VICTORIA MANDARI
2. FRANCIS STOLLA
3. LAU KEGO MASHA ambaye amejitoa jana kumsapoti Tundu Lissu.
4. GODWIN MWAPONGO
5. TUNDU LISSU

Tuwe pamoja kuwaletea yote yanayojiri kutoka ukumbini Arusha International Conference Centre (AICC).

==========

--UPDATES--

Mawakili wameshaanza kuwasili ukumbini. Baada ya mawakili wote kuwasili ukumbini kura zitapigwa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi wa AICC ukaguzi mkubwa sana unafanyika huwezi kuingia kama huna kitambulisho bado mawakili wanaingia kwa ajili ya zoezi la kupiga kura.

Zoezi la kupiga kura bado linaendea mawakili wanaendelea kupiga kura za kumchagua Raisi wa Tanganyika Law Society. (TLS) . Linatarajiwa kumalizika Saa 4:00 asubuhi leo.

Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika mchakato wa kuanza kuhesabu kura unaanza.
Zoezi la kupiga kura limeshaanza kumalizika.

Kupiga kura kumemalizika sasa hivi ni zoezi na kuhesabu kura linaendelea mpaka saa nane mchana mshindi atatangazwa.

Mawakala wakiwa wamebeba kura kuzipeleka sehemu maalumu ya kuhesabu.

Uchaguzi wa TLS kwasasa umefikia hatua ya tatu ya kuhesabia kura!

Tayari mawakala wameingia ndani ya vyumba vya kuhesabia kura. Vyumba hivi ni vinne cha kwanza ni cha uraisi, makamu wa Raisi, mhasibu na wajumbe wa baraza.

Mawakala: Uraisi Wakili msomi Kaunda na makamu wa raisi ni John Malya.

Inategemewa mpaka saa nane matokeo yatakuwa tayari!

Mawakili wamerudi ndani ya ukumbi wa Simba Hall AICC tayari kusubiria matokeo
Bado muda mfupi matokeo yatatolewa yote.

*Nafasi ya Makamu wa Raisi wa TLS Godwin Mwapongo ameshinda.
*Nafasi ya urais Tundu Lissu ameshinda kwa asilimia 88

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE