March 20, 2017

 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema endapo atashindwa kusimamia uhuru wa habari na vyombo vya habari nchini atakuwa hafai kubaki kwenye nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa ameshindwa majukumu yake katika nchi huru.Nape ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia na kulaani kitendo kinachodaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, cha kuvamia chombo cha habari cha Clouds, akiwa na askari wenye silaha na kukifananisha kitendo hicho na kuinajisi taaluma ya habari.
Waziri huyo amesema amezoea kuona matukio kama hayo yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwa bunduki lakini kwa nchi yetu si jambo jema kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki mkononi."Tumezoea kuona matukio haya yanatokea kwenye nchi ambazo zimepinduliwa kwenda kwenye vyombo vya habari na mabunduki si sawa, kwa jambo hili tunataka kutenda haki tumsikilize Mkuu wa Mkoa ili tujue kwanini amefanya jambo hili". Alisema Nape
Kufuatia tukio hilo Waziri Nape ameunda tume yenye wajumbe takribani watano itakayoenda kumhoji Makonda na kutoa mrejesho wa kazi hiyo ndani ya masaa 24 ikiwa imeeleza sababu maalum kutokea kwa tatizo hilo.
 

Dkt. Reginald Mengi
Pamoja na hayo Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Dkt. Reginald Mengi amesema hawezi kutoa lawama kwa mtu yoyote mpaka pale ukweli utakapofahamika japokuwa ameonekana kukerekwa.
"Kwetu sisi hili ni jambo ni la hatari sana, linatuogopesha na linatishia maisha ya waandishi wa habari". Alisema Dkt. Mengi
Kwa upande mwingine Mengi amewasihi waandishi wa habari kutokuwa waoga kwa jambo lolote wanalopambana nalo ila wanachopaswa ni kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa.

Related Posts:

  • Slaa amfagilia Magufuli, aisifu ACT kupambana na ufisadi Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema anamkubali kwa asilimia 90 mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akisema anafaa kwa nafasi hiyo kwa kuwa ni jasiri na ana uwezo wa kup… Read More
  • New Audio| King Kapita_ Vizabizabina| Download hapa Mwana muziki mwenye kipaji cha kukidhi haja toka nchini Tanzania King Kapita, amekuletea tena ngoma yake mpya kabisa aliyomshirikisha Cannibal Shaitta toka nchini Kenya wimbo unaitwa vizabizabina, wimbo ambao umefany… Read More
  • Kauli ya mgombea Urais kwa tiketi ya TLP, baada ya Mrema kumuombea kura Magufuri Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai kuwa … Read More
  • Lowassa afunika Karatu Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbowe, Mjini Karatu, Mkoani M… Read More
  • lowassa aiteka Tarime Vijana wa Mjini Tarime wakiongoza mapokezi ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, alipowasili mjini Tarime kwa Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 10, 2015.… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE