March 30, 2017

 

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye,aliyeondolewa madarakani mapema mwaka huu, amekamatwa Ijumaa hii.Kwa mujibu wa jaji, kukamatwa kwa Bi. Park kumetokana na hofu kuwa anaweza kujaribu kuharibu ushahidi wa makosa anayotuhumiwa. Waendesha mashtaka walitangaza Jumatatu kuwa walikuwa wakifuatilia kukamatwa kwake kwa mashtaka yanayohusiana na kutumia vibaya madaraka, ufisadi na kuvujisha taarifa muhimu.Park alikuwa ameshikiliwa kwa muda katika ofisi maalum za mwendesha mashtaka wa Seoul. Amepelekwa kwenye kituo cha kizuizi cha Seoul Ijumaa hii ambako mshirika wake Choi Soon-sil na watu wengine mashuhuri wanaohusishwa na mashtaka hao akiwemo mrithi Samsung, Lee Jae-yong wanashikiliwa pia.Park bado hajasomewa mashtaka rasmi. Aliondolewa madarakani March 10 baada ya mahakama ya katiba kuamua kumuondoa kutokana na madai ya ufisadi

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE