March 18, 2017

  

Serikali ya Tanzania imekubali ombi la kuipatia Kenya madaktari 500 watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba hasa baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao, baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Wizara ya Afya kutoka Kenya uliotumwa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta.Kiongozi wa ujumbe huo ambaye ni Waziri wa Afya wa Kenya Dkt. Cleopa Mailu amemueleza Rais Magufuli kuwa, baada ya kutokea mgomo wa madaktari pamoja na uamuzi wa nchi hiyo kugatua madaraka katika sekta ya afya, imebainika kuwa nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa madaktari ambao hauwezi kumalizwa kwa kutegemea madaktari wanaosomeshwa nchini humo na badala yake wanahitaji madaktari kutoka nje ya nchiWaziri Mailu aliyeongozana na Gavana wa Kisumu Jack Ranguma amesema Kenya ipo tayari kuwalipa stahili zote madaktari 500 watakaopewa na Serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mishahara na nyumba za kuishi.Kwa upande wake waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema Wizara yake ipo tayari kutoa madaktari hao haraka iwezekanavyo kwa kuwa Tanzania inao madaktari wengi wazuri ambao wamemaliza masomo na hawajapata ajira na wengine wamemaliza mikataba yao ya kazi na bado wana uwezo wa kufanya kazi.
“Kwa hiyo nitoe wito kwa madaktari wote Tanzania ambao hawapo katika utumishi wa umma, hawapo katika hospitali teule na ambao hawapo katika hospitali za mashirika yasiyo ya kiserikali wanaolipwa na Serikali, waombe nafasi hizi". alisema waziri Mwalimu

Related Posts:

  • Wanawake waombwa msamaha wanawake wakifanya maandamano kuadhimisha siku ya wanawake duniani nchini Indonesia   Kampuni inayotengeneza nguo za riadha nchini Indonesia, imeomba msamaha, kwa kuuza t-shat… Read More
  • Mtatiro: Nitagombea Ubunge Segerea   Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala … Read More
  • Chinja chinja wa IS alikuwa mlevi   Mohammed Emwazi ,mtu ambaye alibadilika na kuwa ''chinja chinja'' wa kundi la islamic state kwa jina 'jihad John' Mohammed Emwazi, alifurushwa kutoka nchini Tanzania kwa kuwa mlevi na mtu anayetoa matusi.,afisa m… Read More
  • Rais Kikwete ajivunia kuwabeba wanawakeRais Jakaya Mrisho Kikwete amesema anajivunia kuona anamaliza muda wake akiwa amefanikisha kujenga msingi imara ya kuwawezesha na kuwapa nafasi wanawake katika ngazi za uongozi na hivyo kuwataka viongozi wajao waendelee kuwap… Read More
  • Ubunge Morogoro Mjini, hatimaye Maharagande avaa gwanda rasmi   Maharagande akipokea fomu za kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge morogoro mjini kutoka kwa katibu kata ya Sultani Area Amin Kabwanga katikati, wanaoshuhudia tukio hilo kushoto ni M/kiti CUF  Moro… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE