April 23, 2017

 
Baada ya muingizaji wa filamu, Yusuph Mlela kuomba pambano la ngumi na rapa Nay wa Mitego, rapa huyo amemjibu muigizaji huyo kwa maneno ya kejeli.
Wawili hao waliingia kwenye bifu hilo baada ya Nay wa Mitego kuwaita wasanii wa filamu ‘matahira’ kisa kuandamana kupinga biashara ya filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi.
Rapa huyo amedai hawezi kupigana muigizaji huyo huku akimkejeli kwa kumuita ni mwanamke.

“Nasikia kuna mwanaume/mwanamke yupo Bongo Movie anataka kupigana na mimi, bahati mbaya mimi sipigani na mwanamke hata baba yangu aliniambia mwanamke hapigwi,” alisema Nay kupitia video iliyosambaa mtandaoni.
Aliongeza,

”Naona kuna watu wanashadadia hili suala kwamba tupigane, mimi siwezi kupigana naye labda nitafutiwe mwanaume mwenzangu ili tutengeneze hela lakini kunipiganisha na mwanamke ambaye wamepoteza marinda hapana. Baada ya kutangaza anataka kupigana na mimi Bongo Movie wenzake walinipigia simu wakaniambia achana na huyo mtu ni mwanamke mwenzao alishapoteza marinda,”
Baada ya maneno hayo ya kejeli, Mlela amerudi upya na kusisitiza bado anahitaji pambano na rapa huyo ili amshikishe adabu.

“Nay wa Mitego mimi nimelelewa vizuri na familia yangu ndio maana mambo ya matusi sijazoea ingawa nina uwezo mkubwa niliopewa na mungu baba wa kupambana na matamshi hayo. Kikubwa acha woga, kama shida yako ni pesa huyu aliyepoteza marinda si ndio itakuwa rahisi tu?. Kwangu mimi PESA SiO KILA KITU MUNGU NDIO KILA KITU. Nikuchape au nikuchape (uwezi) PESA ZOTE UTACHUKUA WEWE MIMI SIITAJI ATA SHILINGI MIA. Nay APA RINDA LIPO tena LA ZIGIZAGA uliza vizuri sio Kwa niliowatumia kama dustbin kupitisha siku….sitobishana na wewe tena coz akili yako ya kutaka sifa ni fupi.. eti unakataa movie wakati wewe mwenyewe unafanya movie au ujui kama izo video zako ni movie na TAIFA likiwa na utaratibu mzuri wa kazi za wasanii pia utafaidika…Acha maneno NJOO kwenye stage ili tuheshimiane…samahani Kwa mashabiki zangu ninaowakwaza Kwa hili. #LINDALIPO TENA LA ZIGZAG HAHAHA HAHAHA ,” aliandika Mlela Instagram.

  


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE