Binadamu anayekadiliwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi, Emma Morano amefariki dunia akiwa na miaka 117 huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.
Emma amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwake Kaskazini mwa nchi ya Italia ambapo taarifa ya kifo chake ilithibitishwa na daktari wake Carlo Bava.
Daktari huyo alisema baada ya kugundua kuwa Emma amefariki dunia alitoa taarifa kwa mwangalizi wa Emma na baada ya hapo familia ikapewa taarifa kuwa amefariki.
Dk. Bava alisema Emma amefariki dunia akiwa kwenye kiti kinachotumiwa na walemavu akiwa katika eneo la Verbania lililopo
karibu na Ziwa Maggiore.
karibu na Ziwa Maggiore.
Aidha daktari wake alisema mara ya mwisho kumtembelea ilikuwa siku ya Ijumaa na moja ya mambo aliyomwambia ni kumshukuru kwa kumhudumia kwa kipindi chote ambacho amekuwa daktari wake huku akiwa amemshika mkono.
Emma Morano alizaliwa Novemba 29, 1899 na ni mmoja wa watu ambao wanatajwa kuishi kwa muda mrefu zaid
0 MAONI YAKO:
Post a Comment