April 13, 2017

  
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi 8 wameuawa na majambazi huko Jaribu Kibiti Mkoani Pwani.
Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.
Imeelezwa kwamba majambazo hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.
Habari zaidi tutawaarifu baadaye kadiri tutakavyozipata.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE