Prof. Musa Assad
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa
Assad, imebaini kuwapo kwa matumizi mabaya ya msamaha wa kodi wa
shilingi bilioni 3.46, uliotolewa kwa walengwa wawili walioagiza jumla
ya magari 238 mwaka wa fedha wa 2015/16.
Akiwasilisha
ripoti ya matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016
katika mkutano wa saba na kikao cha saba cha Bunge, Prof. Assad
amesema, msamaha huo wa kodi ulitolewa, lakini magari hayo yalisajiliwa
kwa majina ya watu tofauti na wale waliopewa msamaha.
Hata hivyo, amesema walengwa wote
waliopewa msahaa huo walikana kuhusika na magari hayo, hali inayoonyesha
bado kuna uhitaji wa kuboresha udhibiti na ufuatiliaji wa masuala ya
misamaha ya kodi.
Katika udhibiti wa misahaha ya mafuta
yanayoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya migodi, Prof. Assad
amesema katika ukaguzi walioufanya Mei 31, mwaka jana, wamebaini lita za
mafuta 4,248,802 yaliyosafirishwa kutoka jijini Dar es salaam kati ya
Oktoba 2014 na Disemba 2015 kwa ajili ya matumizi ya mgodi wa Buzwagi,
Bulyankulu na Geita, nyaraka za uthibitisho hazikuweza kufika vituo
husika na kuonesha mafuta hayo yaliyosamehewa kodi yalitumika tofauti na
makusudi.
Pia hiyo imebaini lita 20,791,072 za
mafuta yenye msamaha wa kodi wa shilingi bilioni 10.17 kwa ajili ya
mgodi wa Buzwagi katika kipindi cha miezi 18 kuanzia Julai 2014 hadi
Disemba 2015, yalisafirishwa kwenda kampuni ya M/S Agreeko mkandarasi
msaidizi ambaye hakuwa mhusika wa msamaha huo.
Kutokana na matumizi hayo mabaya ya
msamaha wa kodi, Prof. Assad ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kufanya uchunguzi wa mafuta yote ambayo hayana ushahidi kama
yamesafirishwa vituo vya uchimbaji madini na kukusanya kodi inayodaiwa
kiasi cha shilingi bilioni 1.599 na kodi ya shilingi bilioni 10.17
iliyosamehewa na kupelekwa kwa wakandarasi wasiohusika na msamaha huo.
Aidha, amesema serikali inatakiwa
kuhakikisha usimamizi unaimarishwa juu ya matumizi ya misamaha
inayotolewa kwa mujibu wa sheria ili kuepuka hasara kwa serikali
kutokana na matumizi mabaya ya misamaha ya kod
0 MAONI YAKO:
Post a Comment