April 22, 2017

  

Watu wasiojulikana wakiwa na bastola wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo. 
Mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF, inadaiwa watu hao waliovamia mkutano huo na kufanya vurugu ni wanachama wa Cuf ambao wanamuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo mkutano huo ulipangwa kufanyika majira ya saa tano za asubuhi katika hoteli ya Vina, Mabibo lakini kabla ya kuanza waliibuka watu hao wasiojulikana wakiwa wamevalia soksi nyeusi usoni kuficha sura zao na kususha kipigo kwa baadhi ya wanachama wa CUF waliokuwepo katika eneo hilo na waandishi wa habari. 
Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE