Baada ya Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kutangaza kuwa kesho atageuza Almasi (Diamond) kuwa Maji baada ya wimbo mpya wa Diamond Platnumz ‘Acha Nikae Kimya’ kumtaja kwenye moja ya Mashairi yake hatimae Diamond amerudi na kuomba msamaha.
Diamond Platnumz ilimulazimu kumuomba radhi askofu huyo maarufu wa Kanisa la Ufufuo na uzima lenye makao yake makuu Eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam kwa kuanza kufafanua kuwa hakumaanisha chocochote kibaya kwa Mzee Gwajima badala yake ni tafsiri mbaya tu ya watu waliousikiliza na kushauri wausikilize vizuri wimbo wake mpya.
“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…”Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆”Ameandika Diamond Platnumz.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment