April 23, 2017

Image result for haji manara 

Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara kutojihusisha na soka kwa miezi 12
Licha ya  kufungiwa mwaka mmoja, Manara amepigwa faini ya Sh milioni 9.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE