
Polisi katika jimbo la Ohio nchini
Marekani wanamtafuta mtu anayedaiwa kufanya mauaji,huku akionyesha moja
kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.
Maofisa katika
mji wa Cleveland wamesema kuwa Steve Stephens anaonekana akionyesha
moja kwa moja mauaji wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima
kupitia Facebook.Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amemtaka Stephens ajisalimishe mwenyewe. Williams alisema kuwa mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni kwake.
Polisi wanasema hawajapata ushahidi madai ya Stephen kuwa amewauwa watu kumi na mmoja.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment