April 07, 2017

Mpaka sasa hali ya sintofahamu imegubika sanaa ya Tanzania baada ya miongoni mwa wanamuziki wa kizazi kipya kuchukuliwa na watu wasiojulikana kisha kutoonekana mpaka sasa,baadhi ya watu wa karibu wanasema kuwa wamezunguka vituo vyote vikubwa hawajaonekana mpaka leo Wasanii kwa umoja wao wakamuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam asaidie kuwapata wasanii hao.
Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika>’Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia’
‘Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma’ – Mwigulu Nchemba Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE