April 02, 2017

 

 ........Mashabiki hao waliwapigia saluti wachezaji wao kwa kujituma na kuipandisha daraja timu yao

 

 Abood akiwasili kwenye benchi la Mawezi



 Abood kulia akizungumza na wachezaji,viongozi na mashabiki wa Mawenzi jana




Na Dustan Shekidele:
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh:Aziz Aboodjana ameipa zawadi ya shilingi laki tatu timu ya Mawenzi Market ya mjini hapa baada ya timu hiyo y kupanda daraja la kwanza.

Timu hiyo ya Mawenzi inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Soko la Matunda la Mawenzi imepanda daraja la kwanza kutoka la pili baada ya jana kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri kwa kuinyuka bila huruma timu ya JKT Oljoro ya Arusha kwa bao 2-0.

Katika mchezo huo wauzamatunda hao waliokuwa na Point 6 ilikuwa ni lazima kushinda mchezo huo ili wafikishike Point 9 na kuwapiku wapinzani wao wanajeshi wa JKT Oljoro walikuwa na Point 8 ambao katika mchezo huo walikuwa wakihitaji sale ya aina yoyote ili wajihakikishie kurejea daraja la kwanza waliloshushwa msimu uliopita baada ya kubainika kupanga matokeo.

Hata hivyo Oljoro licha ya kupokea kichapo hicho nao wamerejdaraja la kwanza kufuatia matokeo ya Sale ya bao 1-1 kati ya Trans Camp  ya Shinyanya iliyokuwa na Point 8 na wageni wao Cosmo Politan ya Dar es salaam iliyokuwa na Point 6.

Hivyo kwa matokeo hayo ya sale ya mchezo huo uliopigwa pia jana kwenye uwanja wa Kambarage Mjini Shinyanga Trans Camp imefikisha Point 9 na Cosmo imefikisha Point 7.

Msimamo wa ligi hiyo ni kwamba Mawezi inaongoza kwa kuwa na Point 9 sawa na Trans Camp lakini Mawenzi inaongoza kwa kuwa na uwiano mzuri wa magori huku JKT Oljoro wakishika nafasi ya tatu kwa kuwa na Point 8 na Cosm inashika mkia kwa kuwa na Point 7.

Kwa mujibi wa kanuni za ligi hiyo ndogo timu tatu za juu zinapanda daraja la kwanza huku timu moja ya mwisho inareje ligi daraja la pili msimu ujao.

Katika mchezo wa jana kati ya Mawenzi na wanajeshi wa JKT Oljoro washindi mawezi wameradhimika kusubiri hadi kipindi cha pili kupata mabao hayo mawili.

Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 65 baada ya beki wa kulia wa timu hiyo Berbato Mgotwa 'Macelo wa Mji kasoro bahari' kuchonga kona iliyokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa wa Oljoro akinyaka hewe.

Dakika 90 mfungaji hodari wa timu hiyo Hamis Mkopi' Mtoto wa Chamwino' alipigia msumali wa mwisho kwenye jeneza la Oljoro kwa kufunga bao la pili na kuamsha shanga kutoka kwa kundi kumbwa la mashabiki wa timu hiyo.


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE