Benki
ya NMB Tanzania imezindua rasmi kituo cha biashara mjini Kahama (Kahama
Business Centre) ambacho kitakuwa kikitoa huduma kwa wananchi wa kanda
ya ziwa ikijumuisha mikoa mitatu ya Shinyanga, Tabora na Kigoma.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke
Bussemaker alisema kituo hicho ni sehemu ya mpango wa NMB kuwasogezea
wananchi huduma bora mahsusi kwa wajasiriamali ambapo pamoja na kufungua
kituo hicho pia itatoa mafunzo kwa wajasiriamali.
“Hili tawi
ambalo tumezindua leo ni sehemu ya mpango wetu wa kuwasaidia
wajasiriamali, muda umefika tunahitaji uhusiano mkubwa baina yetu na
wateja wetu ambao ni wajasiriamali,” alisema Bussemaker.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment