April 26, 2017

Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat. 

Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Bingwa huyo wa taji la Grand slam mara 23 alichapisha picha katika mtandao huo wa kijamii akijiangalia katika kioo akiwa ameandika ujumbe wiki 20 kabla ya kufuta kabla ya wasimamizi wake kuthibitisha habari hizo.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.
''Nilikuwa nikijihifadhia'', alisema.
''Nilikuwa nikiendelea vizuri lakini bahati mbaya picha moja nikaichapisha katika Snapchat''.
Bingwa huyo nambari moja kwa upande wa wanawake anatarajiwa kujifungua majira ya vuli, akisema kua aligundua kwamba ana mimba siku mbili kabla ya mashindano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
 Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake. 
Raia huyo wa Marekani alimshinda dadake Venus katika fainali na kuimarisha rekodi yake ya mataji 23 ya Grand Slam.
''haikuwa rahisi'',alisema. Unasikia habari kuhusu walio na mimba, wanakuwa wagonjwa, na wanachoka''.
''Niwe na mimba au la nilijua kwamba ni lazima nishinde. Kila mara ninapocheza, ninatarajiwa kushinda. Iwapo sishindi zinakuwa habari kubwa zaidi''.



Related Posts:

  • BEI YA VYAKULA YAPANDA DAR   BAADHI ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamelalamikia bei kubwa za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye badhi ya masoko jijini humo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, w… Read More
  • MBASHA AMSHTAKI GWAJIMA stori: Waandishi Wetu Mambo juu ya mambo! mvumo mkali wenye kuogofya unaendelea kutamalaki katika ndoa ya wanamuziki zao la upako wa Injili Bongo, Emmanuel na Flora Mbasha, safari hii ‘topiki’ siyo zile tuhuma za u… Read More
  • PITIA MAGAZETI YA LEO HAPA JAPO KWA UFUPI . Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za… Read More
  • SIKILIZA MAGAZETI YA LEO HII 3 JULY HAPA Kupitia hapa unaweza kuskia  magazeti yakisomwa Redioni  leo July 03 nakuletea kwa ajili ya kusikiliza kilichoandikwa kupitia kurasa mbalimbali za Magazeti na hii ni baada ya kupitia kurasa za mbele na nyum… Read More
  •   Aliyekuwa kiungo wa Yanga SC, Athumani Iddi 'Chuji' akiwa mzoezini na klabu bingwa ya Tanzania Bara, Azam FC asubuhi ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.  … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE