Chama cha ACT Wazalendo kimetuma salamu za rambirambi kufuatia vifo
vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva vilivyotokea leo asubuhi kwa
ajali ya gari lilokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa darasa la saba shule
ya msingi Lucky Vicent ya Arusha.
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika haya machache.
Huu ni Msiba wa Taifa Zima, Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa
majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi, walimu pamoja na
wafanyakazi wa Shule ya awali na msingi ya Lucky Vicent ya Jijini
Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea katika wilaya ya
Karatu mkoani Arusha
ACT Wazalendo tunatoa pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao, ndugu
na jamaa waliopoteza walimu na wafanyakazi wa shule hiyo, pamoja na
watanzania wote kwa ujumla. Pia tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii
wapate kupona kwa haraka.
Mola awalaze pema watoto na ndugu zetu wote waliopoteza maisha katika ajali hii. Msiba huu ni wa Taifa zima.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment