May 19, 2017

Mei 12, 2017 uongozi wa klabu ya Simba ulisaini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.9 za Tanzania kwa muda wa miaka mitano.
Baada ya mkataba huo kusainiwa, mambo mengi yakaanza kuibuka ndani ya Simba na kuanza kuchafua hali ya hewa.
Mo ambaye alikuwa akiisaidia Simba kulipa mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi akaibuka na kuanza kudai alipwe pesa zake, wengine wakaanza kusema huenda mchato wa mabadiliko ya uendeshaji ndani ya klabu hiyo ndiyo yamezikwa rasmi.
Kibaya zaidi ni pale walipoibuka wazee wa Simba na kuanza kuongea kauli ambazo si za kupendeza kuhusu Mo.
Kuona yote hayo yakiendelea, Sports Extra ya Clouds FM ikamtafuta makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange Kaburu ili kutoa ufafanuzi wa mambo yalivyo ndani ya klabu ili kuwatoa wanachama na wapenzi wa Simba katika sintofahamu.
Kaburu alielezea mambo mengi lakini muhimu yalikuwa ni kuhusu mkataba waliosaini na SportPesa, mchakato wa mabadiliko na kuhusu sakata la wazee wa Simba.

Kuhusu SportPesa

Tulisaini mkataba na SportPesa lakini kwa watu wengi waliona ilikuwa ghafla na kudhani huenda kuna kitu kwa namna mkataba ulivyosainiwa lakini ilikuwa imeandaliwa hivyo kwamba mkataba uwe surprise. Haukuja kama ajali, kuna mchakato ulifanyika vizuri na maelewano yalikuwepo lakini hizi taarifa zilifichwa ili siku tukitoka basi iwe ni surprise lakini isieleke tofauti na hivyo.
Suala la SportPesa sio la jana wala juzi, ni tangu mwaka jana walikuja wakaonesha nia tukaongea lakini baadae wakapotea. Kupotea kwao kukatupa nafasi ya kukutana na mfadhili wetu MO tukamwambia tuna shida hatuna uwezo wa kulipa mishahara na tayari tumeshaanza ligi na timu inafanya vizuri, tumejaribu kuhangaika hapa na pale lakini tumekwama.
Akakubali lakini akasema atatukosha kwa sababu hakutaka kuwa mfadhili wala mdhamini, tukasaini mkataba kwamba atakuwa akilipa mishahara, akasema hicho anachotukopesha hatuna uwezo wa kulipa. Akasema kwa sababu tupo kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji, anafurahi kwa hatua hiyo na kama tutafanikiwa kufika huko, atakuwa tayari kuwekeza. Mishahara anayotupa kama mkopo hatutalipa ikiwa tutakamilisha mchakato wa mabaliko ya uendeshaji, na chochote alichotukopesha atahesabu kama sehemu ya uwekezaji wake ndani ya Simba.
Baada ya kusaini mkataba na SportPesa, tukaanza kuona tweets za Mo zikionesha amekasirika, hii ikazua hofu kwa wanachama kwamba Mo anaondoka na anadai pesa na tunaelekea kumaliza ligi huku tukiwa tunakabiliwa na mechi muhimu za mwishoni mwa ligi na fainali ya FA.


Mabadiliko

Tulikutana na Mo na tulimwambia ya kwetu na yeye akatuambia ya kwake, kwa hiyo Simba ni kubwa kuliko Mo, Simba ni kubwa kuliko viongozi na wote tumekubaliana tuangalie Simba inahitaji nini. Mwisho wa siku mkataba wa SportPesa upon a tumekubaliana tuendeleze mchakato wetu wa mabadiliko.
Kiu ya Mo ni kuona klabu inabadilika katika uendeshaji ili kupata wadhamini wengi na wawekezaji wengi ili bajeti iwe kubwa na hapo tunaweza kwenda kuwania mataji ya Afrika.
Suala la mabadiliko ndio kilakitu kwa sababu ndio kiu ya huu uongozi, ni kiu ya wanachama wengi, hili jambo sio kama limeibuka tu, ni jambo la siku nyingi lakini tayari sisi kama viongozi tumeshapewa jukumu na wanachama wetu kupitia mkutano mkuu.

Kuhusu wazee wa Simba

Lazima tukubaliane kwamba hii klabu ina uongozi, taratibu ni bora tufanye mambo kwa kufuata taratibu, lakini kuna kuheshimiana kwa hali ya kawaida. Tumewasikia viongozi waliyoyaongea.
Katiba ya Simba inatambua baraza la wazee, baraza hilo linaundwa na walezi wanne Mo akiwa mmoja wapo (kwa hiyo Mo ni mlezi wa Simba), wadhamini wanne, hao wanane watatafuta wazee wenzao watano na kuunda baraza la wazee.
Kazi kubwa ya baraza la wazee ni kusuluhisha migogoro, kwa hiyo kama wazee nilitegemea wangefanya kazi yao namba moja ambayo ni kusuluhisha migogoro na si kutengeneza migogoro. Sasa hao wazee kwenda hadharani kuanza kutoa kashfa si jambo jema sana.
Uongozi upo n a Simba tuna taratibu zetu za ndani ikiwa ni pamoja na vikao vya ndani, wao kama wazee wangeenda walioona jambo hili halifai wangeenda kwa wazee wenzao wakaliongea ndani kama klabu au kulipeleka kwenye matawi kwa sababu tuna vikao vya kila mwezi kwenye matawi.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE