Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT
uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika
mkutano huo
BENKI
ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati
ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara
pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya kwa lengo la kuwakwamua na kuwainua kiuchumi .
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa
akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti
magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka
wafanyabiashara wote kuitumia.
Mkuu
wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo
katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha
Biashara, Donatus Richard (kushoto).
Alisema
kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya
wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye
mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara,
James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika
kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha
katika kuendeleza biashara zao.
Alisema
Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na
taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara
wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment