May 14, 2017

Udukuzi wa komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu 

Wataalmu wa usalama katika mitandao ya komputa, wanaonya kwamba kunaweza kutokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu wataporudi makazini hapo kesho.
Inakisiwa kuwa komputa zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa Ijumaa.
Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya wanasema walioathirika ni 200,000 katika nchi 150.
Shambulio hilo limeathiri watumizi pamoja na ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, mabenki na huduma za afya.
Shambulio hilo limezuwia komputa kufikia data, na wanadai kikombozi, ili kuacha kuikorofisha komputa.
Uchambuzi uliofanywa na BBC katika akaunti tatu za sarafu ya kidijitali, bitcoin, unaonyesha washambuliaji wamelipwa kikombozi zaidi ya mara 100, jumla ya dola karibu 30,000.

Related Posts:

  • UN: Ugaidi hauna mfungamano na dini maalumu    Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa, ugaidi haufungamani na dini au madhehebu fulani na kusisitiza kwamba viongozi wote wa dini ulimwenguni wanalaani na wanapinga kwa nguvu zao zote vit… Read More
  • UKAWA yatangaza kususia Kura ya Maoni   Vyama vya Siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) leo vimetangaza rasmi kuwa vitasusia kushiriki kura ya maoni, kwa ajili ya kupitisha Katiba mpya April 30, 2015 Vyama vya Sias… Read More
  • Rais Kikwete kulifanyia marekebisho Baraza la Mawziri    Mawaziri wote wa baraza la mawaziri nchini Tanzania wamezuiwa kusafiri kikazi nje ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa ni maandalizi ya kukabidhi ofisi kwa mawaziri wapya ambao wanatarajiw… Read More
  • Watoto wa Hosni Mubarak kuachiliwa   Mahakama nchini Misri imeamrisha kuachiliwa kwa watoto wa kiume wa rais wa zamani Hosni mubarak wakati wanaposubiri kesi yao pamoja na baba yao inayohusu ufisadi. Wakili wa Alaa na Gamal Mubarak anasema kwa anatar… Read More
  • New Audio- Mperampera - Mash J ft Stamina Baada ya kufanya poa sana na wimbo wake wa Rimex ya John iliyoimbwa na yemmy Alade wa Nigeria na yeye kuipa jina la Penny, mwanamuziki toka mkoani Morogoro Mash J, safari hii imekuja tena na wimbo wake mpera mpera alio… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE