
Mwanaharakati msomi nchini Uganda ambaye alikamatwa baada ya kumuita
Rais Yoweri Museveni "jozi ya makalio", hatimaye amepewa dhamana.
Msomi huyo na mwanaharakati maarufu wa haki za wanawake na wasichana
aliwekwa rumande kwa mwezi mmoja na kufunguliwa mashtaka ya kutumia
mtandao vibaya. Alimkosoa Museveni na mkewe ambaye ni waziri wa elimu.
Hata hivyo hakimu ametoa masharti kwa msomi huyo kuhakikisha kwamba
yeye na wenzake hawasambazi taarifa zozote ambazo zinahusiana na kesi
dhidi yake ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii kumvunjia heshima rais
Museveni na mke wake Janet pamoja na utawala kwa jumla.
Dkt Nyanzi akisaidiwa kutembea na maafisa wa mahakama
Kufuatia
mashaka kuwa Stella angekamatwa mara tu baada ya kuachiwa na mahakama,
wafuasi wake walijiandaa kumpokea kutoka kwenye korokoro ya muda ili
kuepusha fursa yoyote kwa waliotarajiwa kumkamata kufanya hivyo.
Walimbeba hadi kwenye gari moja binafsi na likaondoka mahakamani kwa
kasi kubwa kiasi kwamba jaribio la wanahabari kupata angalau kauli yake
halikufua dafu.
Stella anakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya
mitandao ya kijamii kumvunjia heshima rais Museveni na mke wake Janet
Kastaha katika harakati zake za kuitaka serikali itoe pedi za bure za
hedhi kwa wasichana nchini. Rais Museveni alikuwa ameahidi kufanya hivyo
katika kampeni zake mwaka jana lakini mkewe ambaye ni waziri wa elimu
alitangaza baadaye kuwa hilo halingewezekana.





0 MAONI YAKO:
Post a Comment