Malkia wa filamu , Wema Sepetu, Jumanne hii amepanda tena katika
mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam, kusikiliza kesi ya
tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya, ambapo upande wa
Jamhuri umekamilisha upelelezi wa kesi inayomkabili msanii huyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ameahirisha kesi hiyo mpaka June 1,
mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza maelezo ya awali ya upelelezi huo.
Muigizaji huyo, ambaye yupo nje kwa dhamana baada kusota mahabusu kwa
siku 7, anadaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake, kufuatia
msako mkali wa kupambana na dawa za kulevya uliofanywa na ofisi ya mkoa
wa Dar es salaam.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment