Na Mwandishi wa Binzuery, KIGALI
AZAM
FC jana imechapwa mabao 4-2 na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa
kirafiki kujiandaa na msimu mpya Uwanja wa Amahoro, Kigali.
Mabao
ya Rayon yalifungwa na Pierre Kwizera dakika ya 30, Nshuti Savio dakika
ya 49, Muhire Kevin dakika ya 67 na Shassir Nahimana dakika ya 90 na
ushei, wakati ya Azam FC yalifungwa na Yahya Mohamed dakika ya 55 na
Mudathir Yahya dakika ya 42.
Unamkumbuka?
Pierre Kwizera ambaye amewahi kuchezea Simba ya Dar es Salaam
akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Rayon jana
Kocha Iddi Nassor ‘Cheche’ aliyekosa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza ambao bado hawajaripoti kwa sababu mbalimbali, baada ya mchezo alisema uchovu uliwaponza.
“Nadhani ni uchovu, tumekuja kwa basi na baada ya siku moja tunaingia kwenye mchezo. Wenzetu walikuwa vizuri na walijiandaa kikamilifu matokeo yake wametufunga,”alisema.
Kikosi cha Rayon kilikuwa; Ndayishimiye Eric Bakame, Manzi Thierry, Mugabo Gabriel, Munezero Fiston, Niyonzima Olivier, Kwizera Olivier, Nova Bayama, Muhire Kevin, Nahimana Shassir, Kakule Mugheni Fabrice na Nshuti Savio Dominique.
Azam FC; Mwadini Ali/Metecha Mnata dk75, Ismail Gambo/Mohammed Ramadhan dk75, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, David Mwantika, Mudathir Yahya, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, Frank Domayo, Yahya Mohammed/Joseph Kimwanga dk58, Yahya Zayed na Iddi Kipagwile.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment