August 15, 2017

Wakili Tundu Lissu ameukataa ushahidi unaoendelea kutolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam dhidi ya msanii  Wema Sepetu kwa madai wakili wa serikali aliiambia mahakama kuwa ushahidi huo ulikuwepo lakini  haukuwa ndani ya bahasha.

Ushahidi huo uliowasilishwa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali ulipingwa na mawakili wanaomtetea Wema Sepetu akiwemo Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatala
Ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali alipeleka vithibitisho anavyotuhumiwa kukutwa navyo Wema Sepetu na watuhumiwa wengine wawili ambavyo ni misokoto miwili ya bangi ambayo ilikuwa imefungwa katika bahasha.

Katika hoja ya wakili wa serikali kwamba bahasha ndiyo ushahidi aliiondoa baada ya kutakiwa kueleza kilichokuwemo ndani ya bahasha ili kitambulike kama ushahidi.

Baada ya kuondoa hoja hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo Thomas Simba alimwamuru mtoa ushahidi kuifungua bahasha, japo upande wa utetezi uliukataa ushahidi huo kwa madai kuwa ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na vielelezo vingine ambavyo mtoa ushahidi hakuvieleza awali, kikiwemo kitu kilichodhaniwa kuwa ni karatasi nyekundu.

Baada ya kusikiliza hoja hizo hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18 ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya ushahidi huo

Related Posts:

  • Balozi wa S Leone atekwa nyara Nigeria   Naibu balozi wa Sierra leone nchini Nigeria ametekwa nyara. Maafisa wa Sierra Leone's wanasema Nelson Williams alitekwa nyara akiwa katika jimbo la Kaduna. Hata hivyo maafisa wa Nigeria wanasema haijbainika wazi… Read More
  • Abdu Kiba adai wasanii wa WCB wanabebwa na Promo Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB. Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, “Sijafikiria kuimba na msanii kutoka WCB, kwa sababu sijaona anayeimba type ya muziki wan… Read More
  • Video: Tamko la BAVICHA kuhusu kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM Julai 23 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa zuio la mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani … Read More
  • Move ya Kukumbukwa:No Retreat, No Surrender   Hii ni kwa wale wapenzi wetu wa Move mbalimbali ulimwenguni. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu tulishindwa kuwawekea Mfululizo wa Move wazipendazo kutokana na marekebisho ya haapa na pale. Sasa leo hi… Read More
  • Apple kununua Tidal ya Jay Z   Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z Tidal. Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ush… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE