Allikiba
Mkali wa 'Seduce Me' Ally Salehe Kiba, amefunguka na kusema katu
hataweza kuishi maisha ya kuigiza umaarufu kwani anaamini watu ndiyo
waliompokea kipindi akiwa hana kitu hivyo kujikweza ni kuwatengenezea
watu hao hila mioyoni mwao.
Kiba alifunguka hayo wakati akitoa
ushauri kwa wasanii wachanga kwa kuwaambia kwamba hakuna kitu kibaya
kama kuishi maisha ya kuigiza umaarufu kwani yanakuwa siyo maisha yao
halisi.
"Watu wanashindwa kujua kuwa
umaarufu wamepatiwa na watu ambao ni mashabiki zetu sisi. Sasa kuwa na
pesa haimaanishi kuwa uishi kwa kuwakomesha waliokuweka hapo u uishi kwa
kuwatengenezea hila mioyoni mwao hakuna mtu
mwenye pesa. Pesa zote tunazotamba nazo ni za serikali hivyo mtu
anayejifanya kwamba anapesa azifungie ndani aone jinsi ambavyo maisha
yatamuendea. Hata masuala ya kuvimba ni ya kuacha kwani najua tukipata
majanga tutaungana tu."
Alikiba aliongeza kuwa "Mimi
nikisema niishi kistaa ukweli sijui itakuaje, lakini kwa vile naamini
mimi ni Super Star hivyo siwezi ku-act maisha kwa vile naamini yale siyo
maisha yangu ingawa wapo watu wengi ambao wanaigiza maisha hayo.
Naamini kuwa kuna watu wanafanya kufurahisha mioyo yao. Lakini kama ni
umaarufu Mzee Majuto mwenyewe ni Star lakini anaishi maisha yake ya
kawaida sana, maisha ya umaarufu siyo ya kwetu tujaribu kuishi maisha
yetu ya kitanzania.
Akiwaasa wasanii wachanga Kiba amewataka
wasanii hao wajifunze kupitia wakongwe wa zamani kwa jinsi ambavyo
walikuwa wakiishi kwa upendo ikiwa ni pamoja na kusapotiana kwa
kuonyeshana upendo na kushikana mikono.
"Natamani kuona jinsi
ambavyo wasanii wa zamani walivyokuwa wakisapotiana ndivyo iwe kwa
wasanii wa sasa. Mimi ni mkongwe lakini kuna wakongwe zaidi niliowakuta
hivyo hatukua na sapoti ya mitandao lakini love ya kutosha ilikuwepo.
Wasanii wa sasa wanaigiza kuishi ki-staa pamoja na kuvimbiana kwa upande
wangu ningewataka waache kuvimba na waweke nguvu kwenye kazi pamoja na
heshima" Alikiba
0 MAONI YAKO:
Post a Comment