Spika wa Bunge la Ethiopia, Abadula Gemeda, amejiuzulu wadhifa wake huo bila kutoa sababu za maamuzi hayo.
Bw. Abadula ametangaza kujiuzulu kupitia televisheni ya taifa ya nchi
hiyo, ameahidi kutoa sababu za maamuzi hayo katika tarehe ya baadaye.
Hata hivyo watu wengi wanadhani uamuzi wa Spika kujiuzulu ni hatua ya
kupinga jinsi serikali kuu inavyoshughulikia hali ya usalama katika
majimbo ya Oromia na Somali, ambapo watu wengi wameuwawa na maelfu
kuondolewa kwenye makazi yao.Spika wa Bunge ni miongoni mwa wanasiasa muhimu nchini Ethiopia na
uamuzi wake wa kujiuzulu umewashangaza wengi. Kabla ya kuchaguliwa
Spika, Bw. Abadula alikuwa ni Mkuu wa Jeshi, Waziri wa Ulinzi na pia
Mkuu wa Jimbo la Oromia
0 MAONI YAKO:
Post a Comment