Mmoja wa washiriki wa shindano la ‘’SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH’’ Akiwa katika mashine kuonesha ujuzi wake huku jaji mkuu DJ PQ akimsikiliza kwa makini mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika fukwe za Coco.
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua upya msimu wa pili wa ‘’Smirnoff ice black’’ (SIB) Dj search . Kampeni hii ya miezi mitatu itakayolenga kusaka Dj bora.
Lengo jingine la uzinduzi huu alifafanua Ester ‘’Ni kuongeza ufahamu wa kinywaji hicho kwa watumiaji wake kwamba ni kinywaji ambacho kipo tayari kwa kunywa na kuhamasisha kuwa ina ladha ya kipekee ya limao.
“Tunaamini kwa kupitia shindano hili , SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia’’. Ester ametaja mikoa ambayo shindano hilo litafanyika, mikoa hiyo ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Morogoro, and Mwanza kila mkoa kutoa maDj 10 na jumla kuwa maDJ 50, mwishoni watapambanishwa na kupata washindi watatu ambao watapokea zawadi kutoka SBL.
Ester alimalizia kwa kusema “Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwaalika maDj wote na wapenzi wa muziki kujumuika nasi katika shindano hili ili kusherekea kwa pamoja na kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black’’
0 MAONI YAKO:
Post a Comment