
CHAMA kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimeishinikiza serikali kuruhusu
vyombo vya uchunguzi vya kimataifa kuchunguza juu ya tukio la kupigwa
risasi mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria wa chama hicho Tundu
Lissu. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hayo mapema leo hii
kuwa, hawana imani na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchini . Mbowe
pia amedai wameshangazwa na kuondolewa kwa kamera za cctv nyumba ya
waziri iliopo jirani na shambulio la kupigwa risasi kwa mbunge huyo
ambaye afya yake inaimarika.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment