October 22, 2017

 

Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi amefunguka na kusema ameagizwa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwaambia wana Mbeya pamoja na Watanzania kiujumla kuwa wajiandae.   

Joseph Mbilinyi amesema hayo baada ya kumtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi nchini Kenya na kusema kutokana na uimara ambao Tundu Lissu anao amewataka Watanzania kujianda. 
"Nimemtembelea 'Big hommie', Nairobi hospital. Ameniambia nikawaambie wana Mbeya kuwa alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na kuwa mwili wake 'uliovunjwa vunjwa' kwa risasi unazidi kuimarika na atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana Mbeya na Watanzania wote wajiandae, wajiandae, wajiandae" alisema Sugu.
  
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini juzi walimtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya anapopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7, 2017. 

Related Posts:

  • LULU: "ACHENI MUNGU ANIHUKUMU"    Msanii wa Bongo Movie Tanzania, Elizabeth Michael "Lulu" ameamua kuchora tattoo iliyoandikwa "Only God Can Judge Me" chini ya shingo upande wa bega lake la kushoto, baada ua kuona watu wamekuwa wakimhuk… Read More
  • DIAMOND TENA, AMSHUTUMU PRODUCER MANECKY JUU YA .... Diamond Platnumz leo hii amefunguka kuhusu kuvuja kwa ngoma yake "Nikifa Kesho"  ambapo amemlaumu producer na inaonekana sababu ni baada ya yeye kuacha kurecord katika studio hiyo. Bado haijajulikana producer … Read More
  • HATIMAE AGNESS MASOGANGE ARUDI TANZANIA Ikiwa ni wiki chache toka kesi ya video vixen Agnes Gerald a.k.a Masogange ya kutuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kuisha kwa kulipa faini nchini Afrika Kusini na kuwa mtu huru, hatimaye  Jumanne amerejea nyumban… Read More
  • NAY WA MITEGO AHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba si… Read More
  • EPHRAIM KIBONDE APATA AJALI MLIMANI CITY   Ephraim Kibonde akishuka kwenye gari baada ya ajali. . .Akilikagua gari lake.   Trafiki akiwa eneo la ajali.   Gari la Kibonde likiwa eneo la ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City baada ya ajali. &… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE