Inafahamika kuwa msanii wa muziki Bongo Flava,Nassibu Abdul au Diamond Platnumz miongoni mwa biashara anazomiliki ni Chibu Perfume na Diamond Karanga,
sasa ametaja ipi inamlipa kati ya hizi mbili.
Hivi
karibuni akiwa katika media tour nchini Uingereza aliulizwa na Idhaa ya
Kiswahili ya BBC ni biashara ipi inamlipa zaidi na jibu lake lake
lilikuwa; ‘Off course, Diamond Karanga’.
Katika hatua nyingine alizungumzia kinachomsukuma zaidi kufungua
biashara mbali mbali kwa kusema kuwa anataka kutumia muziki wake katika
njia ya kujinufaisha hata pale atakapoacha muziki.
“Unaweza kuwa mwanamuziki lakini ukaweza kufanya vitu vingine katika
misingi bora ukatengeneza ajira kwa wenzako ukatengeneza kitu ambacho
hata kesho na kesho kutwa usipoweza kuimba ukaweza kupata riziki na
familia yako ikanufaika” amesema Diamond.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment