Mwanamitindo Calisah amedai kuwa toka mwaka huu, 2017 kuanza hajawahi kutumia kondomu.
Calisah
amesema kitu hicho si cha kujivunia kwa hata yeye anaogopa kwani
magonjwa ni mengi lakini ndio ukweli uliopo katika maisha yake kwa sasa.
“Nisiongope hilo suala na kila siku namuomba Mwenyenzi Mungu
anisaidie, kusema ukweli dah! tangu huu mwaka umeanza sijavaa kodomu,”
Calisah ameiambia FNL ya EATV.
“Mimi kama mfano wa kuigwa si kamba napotosha watu, ni kwamba
nimekosea nasema kwa kijifunza lakini inshallah sitarudia tena hayo
makosa kwa sababu magonjwa ni mengi,” amesema.
Hivi karibuni Calisah alishindwa kushiriki mashindano ya Mister
Africa International yaliyofanyika Lagos Nigeria, licha ya kutumiwa
barua ya mwaliko.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment