Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anaendelea na
matibabu nchini Kenya amesema kuwa wanaendelea kupigana na watashinda
vita hiyo ya ukombozi wa Demokrasia.
Ameyasema hayo baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa Ladhu alipomtembelea jijini
Nairobi.
“Leo nina furaha sana kwa kupata fursa ya kumtembelea sahib na ndugu
yangu, Tundu Lissu, Nairobi Hospital anakoendelea kupata matibabu baada
ya kupigwa risasi zipatazo 16 mwilini Septemba 7, mwaka huu, ametaka
niwafikishie ujumbe huu,”amesema Jusa
Hata hivyo, Jussa amedai kuwa afya ya Tundu Lissu kwa sasa inaendelea
vizuri sana, hivyo amewaasa watanzania kuendelea kumuombea.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment