December 10, 2017


 
 Klabu ya soka ya Manchester City imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa jiji hilo Manchester United kwenye mchezo wa EPL uliomalizika usiku huu kwenye dimba la Old Traford.
Kwa ushindi huu wa leo Man City imeifikia rekodi ya Arsenal ya mwaka 2002 ya kushinda mechi 14 mfululizo. Wakati huo kocha Pep Guardiola ameendeleza ubabe dhidi ya kocha Jose Mourinho ambapo katika mechi 20 walizokutana Guardiola ameshinda 10 huku Mourinho akishinda 4 na kutoka sare mechi 6.
Kwa upande mwingine Man City wamevunja rekodi ya Man United ya kucheza mechi 40 bila kupoteza katika uwanja wake wa  Old Trafford. Mara ya mwissho Man United kufungwa kwenye uwanja huo ilikuwa Septemba 2016 ambapo ilifungwa na Man City hiyo hiyo.

Katika mchezo wa leo Man City ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao katika dakika ya 42 kupitia kwa kiungo David Silva kabla ya Man United kusawazisha kupitia kwa Marcus Rashford dakika 45 kipindi cha kwanza.
Bao la ushindi la Man City limefungwa na mlinzi Nicolas Otamendi dakika ya 54. Manchester City sasa imepanua wigo wa pointi kileleni ikiwa imefikisha alama 43 huku Man United ikiwa na alama 35 katika nafasi ya pili.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE