Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es salaam na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt Hussein Mwinyi ataongoza kuaga miili hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, wananchi wote wanakaribishwa kuhudhuria kwenye shughuli hiyo.
Mnamo Novemba 8, 2017 askari 14 wa JWTZ waliuawa huku askari wengine 44 wakijeruhiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) walipokuwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment