Kiongozi wa upinzani nchini
Kenya kupitia NASA, Raila Omolo Odinga, amesema yupo tayari kufa ikiwa ndiyo
gharama atakayolipa baada ya kuapishwa kama rais wa wananchi, lakini lazima
haki itendeke.
Raila Odinga ametoa
kauli hiyo alipokuwa kwenye mazishi ya Mbunge wa nchi hiyo Francis Nyenze
katika eneo la Kitui, na kueleza kwamba ataapishwa kuwa rais hata kama
itamgharimu hukumu ya kifo kwa kufanya hivyo.
“Iwapo
kifo ndio gharama ambayo lazima tuilipe kwa haki ya uchaguzi Kenya, na kwamba
hakutakuwa na dhuluma za uchaguzi tena baadaye, tupo tayari kulipa hiyo
gharama, tutaapishwa na wafanye kile wanataka kufanya”, alisikika
Raila Odinga.
Odinga aliendelea kwa
kusema kwamba alishinda uchaguzi wa Agosti 2017 ambao ulifutwa na Mahakama ya
Juu, na kuapa kuendelea kupambana kuleta mabadiliko katika uongozi wa nchi.
“Tulisema
tulishinda uchaguzi na tutaapishwa, tumeonywa kwa hukumu na kifo, nataka
nimwambie Githu Muigai (Mwanasheria Mkuu wa Kenya) na bosi wake, tutaapishwa na
tutaufa”, amesema Odinga.
Hivi karibuni Mwanasheri aMKuu wa Kenya amemuonya Raila Odinga kuendelea na mpango wake wa kujiapisha wakati tayari kuna Rais aliyeapishwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, na kusema kwamba sheria itachukua mkondo wake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment