December 16, 2017


Serikali imewataka wasanii kutengeneza kazi nzuri zenye ubora zinazozingatia maadili
ya Kitanzania ili kuwavutia wawekezaji wengi wanaotaka kudhamini kazi hizo katika
kuziandaa na kuzisambaza.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akizindua Mfumo wa MaxBurudani
ulioandaliwa na Kampuni ya MaxMalipo ambapo ameishukuru Kampuni hiyo kwa
kuamua kuchukua dhamana ya kusambaza kazi za wasanii ili kuondoa kero ya muda
mrefu ya wizi wa kazi za wasanii hao kupitia njia mbalimbali walizokuwa wanatumia
wasanii hao ambazo zilikua zikiwalipa kiasi kidogo.

“Mtengeneze kazi zenye ubora na maadili ambazo hata mkipeleka sokoni zilete sifa chanya kwa jamii na wanaowasambazia”

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE