December 15, 2017

Kituo cha Runinga cha Soundcity TV kimetangaza majina ya wasanii watakaowania tuzo za SoundCity MVP mwaka 2017 ambapo Tanzania imefanikiwa kutoa wasanii 5.
Wasanii hao ni Alikiba, Diamond Platnumz, Aslay, Vanessa Mdee na kundi la muziki la Navy Kenzo ambao hao wamechaguliwa kwenye Kipengele kimoja cha Best Group or Duo ambapo watachuana na makundi mengine kama Sauti Sol, Mi Casa n.k .
Alikiba ambaye mwaka jana 2016 alichukua tuzo hizo kupitia kipengele cha Wimbo bora wa Mwaka ‘AJE’. Mwaka huu Alikiba ametajwa kwenye vipengele kimoja cha wimbo bora wa mwaka ‘Song of The Year’ kupitia wimbo wake wa Seduce Me,
Diamond Platnumz naye mwaka huu ametajwa kwenye kipengele kimoja cha kikubwa zaidi cha ‘Best Male MVP’ ambapo atachuana na wasanii wengine Davido, RunTown, Olamide, Wizkid, 2Baba (2face) wote kutoka Nigeria na wengine ni Sarkodie, Shatta Wale kutoka Ghana na Navio kutoka Uganda.

Vanessa Mdee ametajwa tena kwenye kipengele cha ‘Best Female MVP’ ambapo atachuana na wasanii wenzake wa kike kama Tiwa Savage, Niniola, Yemi Alade na wengine kama inavyoonekana hapa chini.
Aslay naye kwa mara ya kwanza ametajwa kuwania tuzo hizo baada ya kuwa na mwaka mzuri katika career yake na ametajwa kwenye kipengele kimoja cha ‘Best New MVP’ ambapo amepangwa na wakali wengine kama Maleekberry, Mayorkun, Diceailes, SmallDoctor wote kutoka Nigeria, Na Nadia Nakai kutoka Afrika Kusini.
Tuzo za Soundcity MVP zitatolewa Januari 12 mwakani jijini Lagos 
nchini Nigeria

BOFYA HAPA KUPIGA KURA

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE