Eneo ambalo bomba la kusafirishia gesi lilipasuka.
Baadhi ya nguzo za umeme zilizoungua kutokana na moto huo.
Taswira ya eneo husika.
Baadhi ya nyumba zilizoungua.
Mabomba yaliyokuwa ardhini.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya wataalamu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakitafuta ufumbuzi wa tukio hilo.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amewataka wananchi waliokumbwa na athari ya moto iliyotokea jana usiku baada ya kupasuka kwa bomba la kusafirishia gesi, kuwa na subira wakati serikali ikijaribu kutafuta chanzo cha moto huo.
Amesema wananchi wanaofanya shughuli za bishara sehemu ambazo siyo rasmi zikiwemo barabara za treni, kuacha mara moja kwani wanaweza kusababisha athari mbalimbali kama ilivyokuwa katika tukio hilo.
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Francis Lupokela, amesema bomba hilo linadaiwa kupasuka baada ya wafanyakazi wa Dawasco kuwa katika matengenezo ya miundombinu ya kurekebisha mabomba ya maji.
Bomba hilo lilipasuka jana jioni ambapo baadhi ya nyumba zinazozunguka eneo hilo ziliungua.
NA DENIS MTIMA/GPL
0 MAONI YAKO:
Post a Comment