Askari usalama wa Nigeria wamewashambulia
watu aliokuwa wakifanya maandamano wakitaka kuachiwa huru Sheikh Ibrahim
Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo (IMN) na kumuuwa
shahidi mfuasi mmoja wa kiongozi huyo wa kidini.
Wafanya maandamano hao ambao
waliandamana katika maeneo yasiyopungua 50 nchini Nigeria, wamemtaka
Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo atoe amri ya kuachiwa huru Sheikh
Zakzaky. Maandamano hayo yamekabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa
wanajeshi wa Nigeria ambao wamemuua shahidi muandamanaji mmoja katika
jimbo la Kaduna.
Maandamano hayo yamefanyika katika hali
ambayo binti wa kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ambaye
yuko kizuizini amesema kuwa hali ya kimwili ya baba yake ni mbaya na
kwamba serikali hairuhusu kiongozi huyo wa kidini apatiwe matibabu.
Kiharusi kilichompata hivi karibuni
Sheikh Zakzaky akiwa kizuizini kimemzidishia hali mbaya ya kimwili kiasi
kwamba, watu wa karibu na mwanazuoni huyo wamesema kuwa, upo uwezekano
Sheikh Ibrahim Zakzaky akapata ulemavu mkubwa na kupooza viungo vya
mwili na hata kushindwa kuzungumza.
Sheikh Zakzaky alipigwa risasi na
wanajeshi wa Nigeria na kisha akatiwa nguvuni kufautia shambulio
lililofanywa na jeshi la nchi hiyo mwezi Disemba mwaka 2015 katika
Husseiniya ya mji wa Zaria. Karibu wafuasi elfu moja wa mwanazuoni huyo
waliuliwa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika shambulizi hilo.
Yapata mwaka mmoja uliopita Mahakama Kuu ya Nigeria ilikutaja kutiwa
nguvuni Sheikh Zakzaky kuwa ni kinyume cha sheria na kuamuru aachiwe
huru haraka iwezekanavyo. Hata hivyo serikali ya Nigeria ingali
inamshikilia Sheikh Zakzaky.
Ibrahim Suleiman mwanachama wa Harakati
ya Kiislamu ya Nigeria ameashiria upinzani wa mara kwa mara wa serikali
ya nchi hiyo dhidi ya ombi la harakati hiyo na familia ya Sheikh Zakzaky
kwa ajili ya kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu na akasema kuna
uwezekano kwamba kunafanyika njama za kumuua shahidi taratibu Sheikh
Zakzaky.
Nigeria ni nchi yenye idadi kubwa ya
Waislamu barani Afrika na ni miongoni mwa nchi tajiri na zenye maliasi
ya mafuta. Nchi hiyo ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ikidolewa jicho la
tamaa na Marekani na waitifaki wake, hivi sasa inapewa mazingatio
maalumu na baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia ambayo
inafanya jitihada za kujipenyeza na kueneza ushawishi wakee barani
Afrika. Kwa msingi huo nchi hizo za Kiarabu hususan Saudia
zinayausia silaha na kuyaunga mkono nyuma ya pazia baadhi ya makundi ya
wanamgambo nchini Nigeria kwa shabaha ya kuzidisha mashinikizo kwa
Waislamu hususan wale wa Kishia.
Waislamu hao pia wanakabiliwa na
mashinikizo kutoka kwa viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika
siku kadhaa zilizopita baadhi ya wakuu wa kijeshi wa Nigeria
walifanya mazungumzo na viongozi wa Israel na kuomba msaada wa
kuimarisha jeshi na uchumi wa nchi hiyo. Uhusiano huo umekuwa sababu ya
kuongezeka mashinikizo dhidi ya Waislamu wa Nigeria na kukabiliwa na
vitendo vya mabavu na ukandamizaji.
Yusuf Hamza mwanaharakati wa kisiasa wa
nchini Nigeria ameashiria namna Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel
na Saudi Arabia zinavyohofia pakubwa suala la kuenea zaidi madundisho
ya Kiislamu kwa mujibu wa madhehebu ya wafuasi wa Ahlul Bait wa Mtume
Muhammad (saw) huko Nigeria na kusisitiza kuwa: Kuna njama za
wazi ya serikali ya Nigeria inayokusudia kumuuwa shahidi taratibu Sheikh
Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment