
Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amefunguka kwa mara ya
kwanza ikiwa ni mwezi mmoja toka afungiwe na Baraza la Sanaa la Taifa
kujihusisha na shughuli za sanaa kutokana na kudaiwa kutoa wimbo
‘Kibamia’ ambao hauna maadili.
BASATA- wamesema walimfungia msanii huyo baada ya kutakiwa na baraza
hilo kubadili wimbo huo lakini hakufanya hivyo na kila alivyoita
hakuweza kutokea.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatato hii, Roma
akiwa na mwanae, Ivan amesema anawaomba BASATA kumpunguzia adhabu kwani
hali yake ya kiuchumi siyo nzuri.
“Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake
kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira, nyuma ya Roma kuna watu ambao
anawasaidia. Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu
Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,” alisema Roma.
Aliongeza,”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata
najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote
na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda
kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja,
Akiwa katika mahojiano hayo na mtoto wake, Ivan aliulizwa na
matangazaji wakipindi hicho kwanini hakwenda shule, na mtoto alisema
hajaenda shule kutokana na tatizo la ada.
“Sijakwenda shule leo baba hana ada,” alisema Ivan mb
0 MAONI YAKO:
Post a Comment