March 04, 2018

Wanachama wa chama cha Social Democrats (SPD) cha Ujerumani wameridhia chama chao kujiunga kwa mara nyingine tena katika serikali ya mseto na muungano wa vyama vya kihafidhina - Christian Democratic Union (CDU) cha Kansela Angela Merkel na Christian Social Union (CSU), baada ya matokeo ya kura zilizopigwa kwa njia ya posta, zilizoonesha kuwa wameridhia kwa asilimia 66. Matokeo hayo ya kura yatafungua njia kwa serikali iitwayo Muungano Mkuu kati ya SPD, CDU na CSU, ambao umeongoza nchini Ujerumani tangu mwaka 2013. Vile vile, uamuzi huu wa leo unahitimisha mkwamo wa kisiasa wa takribani miezi minne katika taifa lenye nguvu zaidi kiuchumi barani Ulaya.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE