Wakili Msomi Fatma Karume ameshinda nafasi ya Urais wa Chama Cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na kuwa mrithi wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye amemaliza muda wake leo kutumikia nafasi hiyo kama Rais.
Fatma
Karume ametangazwa mshindi baada ya kuwashinda Simba Ngwilimi, Musa
Mwapongo pamoja na Godfrey Wasonga ambao nao walikuwa wakigombea nafasi
hiyo ya Urais wa TLS.
Kufuatia ushindi huo wa Fatma Karume Mbunge wa Kigoma Mjini kwa
tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameweza kuwatumia ujumbe
wa pongenzi na kusema kuwa wao watashirikiana nao kuhakikisha utawala wa
sheria na Katiba unafuatwa nchini.
"Nawapongeza sana Fatma Karume na Dkt. Rugemeleza Nshala
kwa kuchaguliwa kuwa Rais na Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika ( TLS ). Ushindi wenu ni ushahidi wa imani kubwa waliyonayo
wanasheria nchini. Tutashirikiana Katika kuhakikisha utawala wa sheria
na Katiba unafuatwa nchini" alisisitiza Zitto Kabwe
0 MAONI YAKO:
Post a Comment