
Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART)
imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa
11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la
Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea
kunyesha
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa na
kusema wamechukua maamuzi hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita
juu ya daraja la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam hali ambayo
inahatarisha usalama wa abiria na vyombo vya usafirishaji.
"Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara - Morroco,
Kimara - Magomeni Mapipa, na Gerezani - Muhimbili. Huduma kamili
zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa", amesema Bugaywa.Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao umejitokeza.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment