August 18, 2018

Image result for kofi annan  
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amefariki Dunia.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Kofi Annan amefariki leo baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Annan alikuwa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo.
Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa mbaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.
Muhula wa Annan kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikumbwa na vita vya Iraq na janga la virusi vya HIV na Ugonjwa wa ukimwi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE