
Malema aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na EFF, ambapo aliongelewa mambo mbalimbali ikiwemo ujumbe wa Rais wa Marekani kwenye mtandao wa Twitter kuhusu marekebisho ya sheria ya ardhi Afrika Kusini.
"Tunatakiwa kuzalisha lugha moja ambayo itatumika kwenye bara zima. Kwa mfano Kiswahili, kinaweza kukuzwa ili kitumike barani kote" alisema Malema.
Lugha ya kiswahili ni lugha inayotumika sana barani Afrika, ambapo kinatumika sana Afrika mashariki na kati. Ni lugha rasmi kwa nchi ya Tanzania na Kenya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment