DC wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wote wanaoendesha
shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na
Kazimzumbwi wilayani humo kuondoka mara moja kabla hajatumia nguvu.
Akiwa
ndani ya msitu wa Ruvu Kusini Jokate amezindua operesheni ya siku 6 ya
kuwaondoa wavamizi na kuipa jila la “Operesheni Jokate”.
Jokate
ameyafanya hayo jana Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako
alienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa
Misitu (TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo.
Amesema
lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao hawataki kufuata
sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu Kusini.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment