WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Harrison Mwanyembe, amezitaka kampuni za visimbuzi za DSTV,
Azam na Zuku kwenda kwenda Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wapewe
utaratibu wa kurusha chaneli za ndani za bure kama wamevutiwa na soko
hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo Jumanne Agosti 14 Mwakyembe amesema licha ya mikataba
ya kampuni hizo kutoruhusha kurusha chaneli hizo lakini wamekuwa
wakizirusha na kuwatoza wananchi gharama ili kuzipata.
“Kama hawa wenzetu wana hamu sana na
soko hili la ndani wasitumie njia za chini chini waende TCRA wapewe
utaratibu wa namna wa kuupata,” amesema Mwakyembe.
Alizitaja baadhi ya chaneli ambazo
zinapaswa kupatikana bure kupitia visimbuzi mbalimbali ni pamoja na TBC,
Star TV, ITV, Channel Ten na EATV na kusisitiza kuwa TBC ni lazima
irushwe na kila kisimbuzi bila malipo yoyote.
Dk. Mwakyembe amesema pamoja na
ufafanuzi mzuri uliotolewa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
ameamua kulitolea ufafanuzi jambo hilo ili kuondoa sintofahamu kwa
wananchi.
“Naomba nianze kwa kutamka kwamba
maelezo yote yaliyotolewa na Waziri Isack Kamwelwe yanawakilisha majibu
ya wizara yangu,” amesema.
Dk. Mwakyembe pia amesisitiza kuwa
serikali haijafuta leseni za visimbuzi vya Azam, Zuku na Multichoice
Tanzania bali wanawataka kuondoa chaneli ambazo zinatakiwa kurushwa bure
kulingana na matakwa ya mikataba yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment