Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema anahofia usalama wake
kutokana na taarifa alizozipata, akisema kuna mpango wa kumdhuru.
Kiongozi huyo wa upinzani ambaye amekuwa mstari wa mbele katika
kusimamia agenda za muungano wa vyama 10 vya upinzani kuanzia mwishoni
mwa mwaka jana, alieleza kupitia mtandao wa Twitter, akionya wale
walionuia kumdhuru.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Zitto ameandika; “Tunafahamu kuwa
Operesheni Maalumu #Mzizima2 imepewa kibali kutekelezwa. Dhima ‘ Vita ya
Mwisho kuleta Nidhamu kamili’ inataka kinachoitwa kumnyamazisha SAI(
mie huyo). Wakajipange upya Tu. Mungu tu Ndio anaweza kuninyamazisha.
SIOGOPI mwanadamu mwenzangu aslani” alisema katika ukurasa huo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment