RC Makonda akimtolea mfano msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz, amesema kuwa kuna watu kipindi msanii huyo anaugua, walikuwa wanatangaza amefariki dunia, leo amepona na ametoa wimbo wake mpya wa kumshukuru Mungu watu hao wamekaa kimya kama hawajui.
“Ukitaka kujua watu walivyo wa Ajabu tazama leo, Ommy dimpo alikuwa mgonjwa sana na ikafika hatua ya watu kutangaza Amekufa. Leo amerejea tena akiwa na wimbo wa kumshukuru Mungu wamekaa kimya Kama vile siyo wao waliokuwa wana post kumwombea apone. Angefariki tungeona mitandao yote imechafuka RIP Ommy oooh umeenda bado tunakuhitaji. Unafiki huu sijuwi utaisha lini, tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji,“ameandika RC Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Ommy Dimpoz kwa sasa amerejea nchini akitokea Ujerumani alikokuwa akitibiwa kwa takribani miezi miwili.
Tangu aanze kuugua Ommy Dimpoz, RC Makonda amekuwa ni mtu wa karibu kumjulia hali, na kuna kipindi alishawahi kuujulisha umma juu ya afya ya Ommy.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment